2,4-D ICSC: 0033
Aprili 1994

2,4-Dichlorophenoxyacetic acid
CAS # 94-75-7 C8H6Cl2O3
RTECS # AG6825000 Masi ya molekuli: 221.0
UN # 2765
EC # 607-039-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na vioksidishaji.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko ikiwa michanganyiko vyenye vimumunyisho huweza kuwaka/kulipuka.


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika. Udhaifu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinayokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-36/37/38
S: (2-)-36/37
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G53c
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4-D ICSC: 0033
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU PODA NYEUPE, ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha kloridi hidrojeni na fosjini. Dutu hii ni asidi dhaifu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 mg/m3 (kama TWA) (ACGIH 1993-1994)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu, (tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana kabla ya kuchemka
Kiwango myeyuko: 138°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.6
Umumunyifu katika maji: hakuna
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.81
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
2,4-D klorofenoksi ambayo ni kiuwadudu, ni kikundi kilichoainishwa kuwa na uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za sumu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005