CYCLOHEXANETHIOL ICSC: 0032
Aprili 2004

Cyclohexyl mercaptan
CAS # 1569-69-3 C6H11SH
RTECS # GV7525000 Masi ya molekuli: 116.2
UN # 3054
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu, dioksidi kaboni, poda.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 43°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 43°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kusinzia. Kutapika. Udhaifu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GFI-II
Msimbo wa NFPA: H ; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na kinakisishaji, metali, vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CYCLOHEXANETHIOL ICSC: 0032
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu pamoja na dioksidi sulfuri (tazama ICSC0074). Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, kinakisishaji na metali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo huweza kuleta kupungua kwa fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 158°C
Kiwango myeyuko: -118°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.98
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.0
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.04
Kiwango cha kumweka: 43°C c.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kiwango cha joto cha kuweza kuwaka yenyewe havipo katika maandiko. Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005