| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Mnyunyizo wa maji, poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 86°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 86°C, uingizaji hewa.
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kichefuchefu. Kutapika. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T R: 24/25-34 S: (1/2-)-36/37/39-45 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G61b Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 0; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO RANGI, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA HEWA NA MWANGA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5 ppm (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 2000). Ainisho ya MAK H,3 (1999) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake au erosoli kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mfumo wa moyo na mishipa, mapafu, mafigo na ini, kusababisha kudidimiza utendaji wa mfumo mkuu wa neva, kutoweza kupumua na vidonda vya tishu. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kupungua kwa fahamu na kifo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa na mfumo mkuu wa neva. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 202°C Kiwango myeyuko: 35°C Uzito wiani: 1.02 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 1.9 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 15 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7 |
Kiwango cha kumweka: 86°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 559°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1 (ifikapo 150°C) -? Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.94 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||