2-CHLORO-1-NITROBENZENE ICSC: 0028
Oktoba 2002

o-Chloronitrobenzene
o-Nitrochlorobenzene
1-Chloro-2-nitrobenzene
CAS # 88-73-3 C6H4ClNO2
RTECS # CZ0875000 Masi ya molekuli: 157.6
UN # 1578
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na dutu ziwakazo.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1578-S
Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 1;
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-CHLORO-1-NITROBENZENE ICSC: 0028
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO HADI KIJANI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (oksidi za nitrojeni, klorini - ona ICSC0126, kloridi hidrojeni - see ICSC0163, fosjini - ona ICSC0007). Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. Tazama Vidokezo. BEI issued (ACGIH 2004).
MAK: skin absorption (H); kuingia kupitia kwa ngozi (H); <13428020?Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu na ini kusababisha kufanyika kwa methemoglobini, anemia na kuharibika kwa ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 246°C
Kiwango myeyuko: 33°C
Uzito wiani: 1.4 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.6
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.4
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03
Kiwango cha kumweka: 124°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 487°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.15-13.1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.24
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
TLV (kama para-nitrochlorobenzene): 0.1 ppm (ngozi), dutu hii iko daraja A3 ikihakikisha kusababisha kansa kwa wanyama (ACGIH 2004). Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005