CHLOROFORM ICSC: 0027
Aprili 2000

Trichloromethane
Methane trichloride
Formyl trichloride
CAS # 67-66-3 CHCl3
RTECS # FS9100000 Masi ya molekuli: 119.4
UN # 1888
EC # 602-006-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Tazama Vidokezo. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Ngozi kavu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kutapika. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-38-40-48/20/22
S: (2-)-36/37
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1888
Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho namaunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali.). Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CHLOROFORM ICSC: 0027
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu (kloridi hidrojeni ICSC0163, fosjini ICSC0007 na mafusho ya klorini ICSC0126). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi kali, vioksidishaji vikali, baadhi ya metali kama vile alumini, magnesiamu na zinki, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm kama TWA; A3; (ACGIH 2004).
MAK: 0.5 ppm, 2.5 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 4; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva ini na mafigo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 62°C
Kiwango myeyuko: -64°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.48
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.8
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 21.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.12
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.7
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.97
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Huungua kutoka na ongezeko la kiasi kidogo cha dutu inayoweza kuwaka au kuzidi kwa kiasi cha oksijeni hewani. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005