CARBON TETRACHLORIDE ICSC: 0024
Aprili 2000

Tetrachloromethane
Tetrachlorocarbon
Tetra
CAS # 56-23-5 CCl4
RTECS # FG4900000 Masi ya molekuli: 153.8
UN # 1846
EC # 602-008-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-40-48/23-52/53-59
S: (1/2-)-23-36/37-45-59-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1846
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, metali (tazama Hatari za Kikemikali). Uingizaji hewa kwenye sakafu. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CARBON TETRACHLORIDE ICSC: 0024
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu. (kloridi hidrojeni ICSC0163, mafusho ya klorini ICSC0126, fosjini ICSC0007). Humenyuka pamoja na baadhi ya metali kama vile alumini, magnesiamu, zinki, kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA, 10 ppm as STEL; (ngozi); A2; (ACGIH 2004).
MAK: 0.5 ppm, 3.2 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 4; Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo na mfumo mkuu wa neva, kusababisha kupoteza fahamu. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 76.5°C
Kiwango myeyuko: -23°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.59
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.1 mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 12.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.3
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.64
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa tabaka ya ozoni.
VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005