CARBON DISULFIDE ICSC: 0022
Oktoba 2000

Carbon disulphide
Carbon bisulfide
Carbon sulfide
CAS # 75-15-0 CS2
RTECS # FF6650000 Masi ya molekuli: 76.1
UN # 1131
EC # 006-003-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kutapika. Udhaifu. Ukereketwaji. Mauzauza.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Usimpe chochote cha kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, T
R: 11-36/38-48/23-62-63
S: (1/2-)-16-33-36/37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1131
Msimbo wa NFPA : H 3; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji, vyakula na malisho. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CARBON DISULFIDE ICSC: 0022
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na nyuso za moto na hewa huzalisha mafusho yenye sumu ya dioksidi za sulfuri (tazama ICSC 0074). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm; (ngozi); BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: 5 ppm, 16 mg/m³; kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Mfiduo wa 200 hadi 500 ppm huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa na mfumo wa neva, kusababisha kuziba kwa mishipa ya damu kwenye moyo na kusababisha ugonjwa wa moyo, kuvimba kwa neva na ukichaa (coronary heart disease, polyneuritis, psychoses). Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 46°C
Kiwango myeyuko: -111°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.26
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.2
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 48
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.63
Kiwango cha kumweka: -30°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 90°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1-50
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.84
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005