| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Ongezeko la msukumo wa damu. Tachycardia.
|
Uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1013
|
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI, ISO HARUFU HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 2000°C huzalisha monoksidi kaboni yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi kali na metali za alkali. Poda za metali kama vile magnesiamu, zirconiamu, titaniamu, alumini, kromiamu na manganisi zinaweza kuwaka na kulipuka zikipata dioksidi kaboni. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5000 ppm kama TWA; 30000 ppm kama STEL; (ACGIH 2004). MAK: 5000 ppm, 9100 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Kuvuta pumzi yenye ukolezi mkubwa wa gesi hii kunaweza kusababisha kupumua kwa kasi (hyperventilation) na kupoteza fahamu. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri umetaboli. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango usablimishaji: -79°C Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 20°C: 88 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 5720 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.5 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Carbon dioxide is given off by many fermentation processes (wine, beer, etc.) and is a major component of flue gas. Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Nambari nyingine za UN: 1845 dioksidi kaboni, mango (dry ice); UN 2187 dioksidi kaboni, gesi oevu iliyobanwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||