CADMIUM ICSC: 0020
Aprili 2005

CAS # 7440-43-9 Cd
RTECS # EU9800000 Masi ya atomi: 112.4
UN # 2570
EC # 048-002-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika umbo la unga na huweza kuwaka yenyewe katika umbo la piroforiki Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na moto au asidi.
Mchanga mkavu, poda maalum. USITUMIE vitenzi vingine.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama.
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 45-26-48/23/25-62-63-68-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Isodhurika kwa moto. Kavu. Weka katika gesi ajizi. Kinachotenganishwa na moto vioksidishaji asidi, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CADMIUM ICSC: 0020
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MABONGE METALI LAINI BLUU-NYEUPE AU PODA KIJIVU MALLEABLE. HUGEUKA IVUNJIKAYO INAPOFIDULIWA NA JOTO (80°C). HUBADILIKA RANGI INAPOFIDULIWA NA HEWA YENYE UNYEVU.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na asidi kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001). Poda ya metali humenyuka na vioksidishaji, azidi hidrojeni, zinki, selenium au tellurium, kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (vumbi) 0.01 mg/m³; (sehemu pumuzi) 0.002 mg/m³; kama TWA; A2; BEI imetolewa; (ACGIH 2005).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembeya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mafusho inakera njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye mafusho kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta hewa yenye mafusho kunaweza kusababisha homa ya metali. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa chembe za vumbi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo kusababisha kuharibika kwa figo. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 765°C
Kiwango myeyuko: 321°C
Uzito wiani: 8.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Jotoridi la kujiwasha: (poda ya metali kadimi) 250°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji, povu, dioksidi kaboni na halons. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Cadmium pia inapatikana katika umbo la piroforiki (EC No. 048-011-00-X), ambayo ina alama za ziada za utambulisho za EU F, R: 17, na S: s 7/8 na 43. Namba za Umoja wa Mataifa na kundi la kufungashia litabadilika kulingana na umbo halisi la dutu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005