| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji, poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kusinzia. Kiwaa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Tazama Ngozi.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: F+, T R: 45-46-12 S: 53-45 Angalia: [D] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1010 Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Baridi. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. Mvuke wa 1,3-butadiene hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto vya matangi ya kuhifadhia, kuziba kwa matundu hufuatia. HATARI ZA KIKEMIKALI: Katika hali mahsusi (mgusano na hewa) dutu hii huweza kutengeneza peroksidi na kuanzisha upolimishaji lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kupata joto kwa athari ya moto au mlipuko. Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa shaba na aloi zake (tazama Vidokezo). Dutu hii hutengana kwa mlipuko ikikanzwa na kushinikizwa. Humenyuka kwa nguvu ikiwa na vioksidishaji na dutu nyingine nyingi, kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 ppm kama TWA; A2 ; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 1: Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 2; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha lowering of consciousness. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri uboho, kusababisha lukemia. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. Huweza kusababisha uharibifu wa kijeni unaorithika kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -4°C Kiwango myeyuko: -109°C Uzito wiani (maji = 1): 0.6 Umumunyifu katika maji: hakuna (0.1 g/100 ml) Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 245 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.9 |
Kiwango cha kumweka: -76°C Jotoridi la kujiwasha: 414°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1-16.3 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.99 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Bomba la gesi hii lisizidi kuwa na 63% ya shaba. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||