BENZYL CHLORIDE ICSC: 0016
Oktoba 2001

alpha-Chlorotoluene
(Chloromethyl)benzene
Tolyl chloride
CAS # 100-44-7 C7H7Cl / C6H5CH2Cl
RTECS # XS8925000 Masi ya molekuli: 126.6
UN # 1738
EC # 602-037-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 67°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 67°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kichefuchefu. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kizunguzungu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Inayotoza machozi. Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kutapika. Mchomo nyuma ya mfupa wa kidari.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika chombo isiyo metali vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-22-23-37/38-41-48/22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1738
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 1;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BENZYL CHLORIDE ICSC: 0016
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha kwa kuathiriwa na metali zote isipokuwa nikeli na risasi, huku ikitoa mafusho babuzi (kloridi hidrojeni - ona ICSC 0163), kwa athari ya moto au mlipuko. Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu na babuzi (kloridi hidrojeni). Humenyuka kwa nguvu ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; A3 (ACGIH 2001).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kunyunyiza kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho. Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake au erosoli yake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kupoteza fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo kusababisha vidonda vya tishu. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 179°C
Kiwango myeyuko: takribani -43°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.1
Umumunyifu katika maji: hakuna (<0.1 g/100 ml)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 120
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.4
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 67°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 585°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1-14.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005