CHRYSOTILE ICSC: 0014
Machi 1999

Asbestos, chrysotile
White asbestos
Serpentine chrysotile
CAS # 12001-29-5 Mg3Si2H4O6 / Mg3(Si2O5)(OH)4
RTECS # CI6478500 Masi ya molekuli: 277
UN # 2590
EC # 650-013-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga ya kupumulia. Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).

Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-48/23
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 9
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90S2590
Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CHRYSOTILE ICSC: 0014
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO NYEUPE, KIJIVU, KIJANI AU MANJANO YENYE NYUZINYUZI.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (Kwa nyusi ndefu kuliko 5 um na uania inayotoshana au zaidi kwa 3:1 kama invyodhamiriwa na utando kwa 400-450 x kwa ukuzaji (membrane filter method at 400-450X magnefication, 4-mm objective, phase contrast elimination) 0.1nyusi/cc kama TWA; A1; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 1; (DFG 2004).
EU OEL: 0.1 nyuzi/cm³ (EU 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mapafu, kusababisha fibrosisi ya mapafu na mesotelioma. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): tazama Vidokezo
Uzito wiani: 2.2-2.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii inastahimili joto mpaka digri 500°C na huchanganua kabisa kwa joto la digri 1000°C. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu asbesto nyingine. Avibest C, 7-450 asbestos, Calidria RG 144, Calidria RG 600, Calidria RG 100, Hooker no.1 chrysotile asbestos, K 6-30, Plastibest 20, RG 600, 5RO4, Sylodex, Cassiar AK, Cassiar A 65, Fritmag, P 3-50 NA P 4-20 ni majina ya kibiashara. Nambari nyingine za CAS: 132207-32-0.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005