ARSENIC ICSC: 0013
Oktoba 1999

Grey arsenic
CAS # 7440-38-2 As
RTECS # CG0525000 Masi ya atomi: 74.9
UN # 1558
EC # 033-001-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na vioksidishaji vikali. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapowekwa kwenye mwalimoto au nyuso zenye joto ni kidogo iwapo katika hali ya poda laini au vumbi.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kukosa pumzi. Udhaifu. (Tazama Kumeza).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Mchomo. kooni na kifuani Mshtuko au kuzimia. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/25-50/53
S: (1/2-)-20/21-28-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-II
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi, halojeni vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ARSENIC ICSC: 0013
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE KIJIVU, KAMA METALI; ISO HARUFU.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali na halojeni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na asidi, huzalisha mafusho yenye sumu (tazama ICSC0222 Arsine).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.01 mg/m³ kama TWA; A1; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo wa moyo na mishipa, mfumo mkuu wa neva na mafigo, kusababisha uvimbe wa tumbo na chango, upungufu wa maji na eletroliti mwilini, ugonjwa wa moyo, mshtuko, degedege na kuharibika kwa figo. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri kiwamboute, ngozi, mfumo wa neva wa pembeni, ini na uboho, kusababisha kugeuka kwa rangi ya asili, ugumu wa ngozi, vitobo vya tenganisho la pua, uvimbe wa neva, kuharibika kwa ini, anemia. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango usablimishaji: 613°C
Uzito wiani: 5.7 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Dutu hii inaweza kuwaka lakini kiwango mlipuko hakikuelezwa katika maandiko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Pia shauriana na Arsenic pentoxide (ICSC0377), Arsenic trichloride (ICSC0221), Arsenic trioxide (ICSC0378), Arsine (ICSC0222).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005