ANTIMONY TRIOXIDE ICSC: 0012
Mei 2003

Antimony sesquioxide
Antimony(III) oxide
Antimony white
Flowers of antimony
CAS # 1309-64-4 Sb2O3
RTECS # CC5650000 Masi ya molekuli: 291.5
UN # 1549 (ona Vidokezo)
EC # 051-005-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kuumwa koo. Kutapika. Maumivu kama kuungua tumboni. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 40
S: (2-)-22-36/37
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-III
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ANTIMONY TRIOXIDE ICSC: 0012
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu. Katika hali fulani, humenyuka pamoja na hidrojeni kutengeneza gesi (stibine) yenye sumu kali sana.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (kama Sb) 0.5 mg/m³ (ACGIH 2003).
TLV: antimoni trioksidi (uzalishaji) A2 (inahisiwa kuwa kasinojeni kwa binadamu); (ACGIH 2003).
MAK: Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2005).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa vumbi ya dutu hii. Tezi zimeonekana katika majaribio ya wanyama lakini huweza isiwe hivyo kwa binadamu (tazama Vidokezo). Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: (usablimishaji kiasi hutokea) 1550°C
Kiwango myeyuko: (ona Vidokezo) 656°C
Uzito wiani: (ona Vidokezo) 5.2/5.7 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 30°C: 0.0014 (hakuna)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 574°C: 130
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa krastashia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kiwango myeyuko kilichowekwa bila kuwepo oksijeni. Uzito hutofautiana kulingana na umbile la fuwele. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Mapendekezo yaliyomo kwenye kadi hii hayahusu mfiduo wa mafusho wakati wa utengenezaji. Tokeo la teknikali la weza kuwa na mchafuko unaoweza kugeusa matokeo kwa afya. Kwa maelezo zaidi ona ICSC0013 Arseniki. Kanuni za UN: nafasi maalumu SP45 inatumika katika namba ya UN 1549 (Hatari daraja la 6.1 na kundi la ufungaji III). Ina maana kuwa antimoni sulfidi na oksidi ambazo zina kiwango kisichozidi 0.5% ya aseni iliyohesabiwa katika uzito haziathiriwi na kanuni hizi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005