ANILINE ICSC: 0011
Machi 2001

Benzeneamine
Aminobenzene
Phenylamine
CAS # 62-53-3 C6H7N / C6H5NH2
RTECS # BW6650000 Masi ya molekuli: 93.1
UN # 1547
EC # 612-008-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 70°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 70°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kupumua kwa shida. Degedege. Ongozeko la mapigo ya moyo. Kutapika. Udhaifu. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-40-41-43-48/23/24/25-68-50
S: (1/2-)-26-27-36/37/39-45-46-63-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1547
Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ANILINE ICSC: 0011
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI KAMA MAFUTA, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA HEWA AUMWANGA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa wa mfumo funge wa zaidi ya 190°C huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (amonia na oksidi za nitrojeni) na mivuke inayowaka. Dutu ni besi dhaifu. Humenyuka kwa nguvu ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali. Hushambulia shaba na aloi zake.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm; (ngozi); A3; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: 2 ppm, 7.7 mg/m³; kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya kiwango cha juu: II(2); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza, pia kama mvuke!

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 184°C
Kiwango myeyuko: -6°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.02
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 3.4
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 40
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.2
Kiwango cha kumweka: 70°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 615°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.2-11
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.94
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005