ALLYL CHLORIDE ICSC: 0010
Oktoba 2004

3-Chloro-1-propene
3-Chloropropylene
Chloroallylene
CAS # 107-05-1 C3H5Cl / CH2=CHCH2Cl
RTECS # UC7350000 Masi ya molekuli: 76.5
UN # 1100
EC # 602-029-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na maunzi yasiokubaliana: tazama Hatari za Kikemikali.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Udhaifu. Kupumua kwa shida. Kutapika. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mchomo. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwanivuli ya usalama au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xn, N
R: 11-20/21/22-36/37/38-40-48/20-68-50
S: (2-)-16-25-26-36/37-46-61
Angalia: [D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1100
Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ALLYL CHLORIDE ICSC: 0010
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha kwa kuathiriwa na asidi joto na peroksidi kwa athari ya moto au mlipuko. Inapowaka hutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu kloridi hidrojeni (tazama ICSC0163). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali na poda ya metali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na maji kusababisha asidi hidrokloriki. Hushambulia plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; 2 ppm kama STEL; (ngozi); A3; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Kuvuta pumzi ya mvuke wa viwango vya juu kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva wa pembeni, mfumo wa moyo na mishipa, mafigo, ini kusababisha kuharibika kwa figo, kuharibika kwa ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 45°C
Kiwango myeyuko: -135°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.94
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.36
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 39.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.6
Kiwango cha kumweka: -32°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 390°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.9-11.2
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.1
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005