ACETALDEHYDE ICSC: 0009
Novemba 2003

Acetic aldehyde
Ethanal
Ethyl aldehyde
CAS # 75-07-0 C2H4O / CH3CHO
RTECS # AB1925000 Masi ya molekuli: 44.1
UN # 1089
EC # 605-003-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Uingizaji hewa. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kuhara. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: F+, Xn
R: 12-36/37-40
S: (2-)-16-33-36/37
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1089
Msimbo wa NFPA: H 2; F 4; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichopozwa. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ACETALDEHYDE ICSC: 0009
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI AU KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na hewa dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha kwa kuathiriwa na asidi na hidroksidi ya alkali pakiwepo na metali katiti (feri) kuna athari ya moto au mlipuko. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji asidi kali, halojeni na amini kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 25 ppm kama STEL; (kiwango cha juu) A3; (ACGIH 2003).
MAK: 50 ppm, 91 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji kusababisha vidonda vya tishu. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 20.2°C
Kiwango myeyuko: -123°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.78
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 101
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.5
Kiwango cha kumweka: -38°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 185°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 4-60
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.63
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005