TETRAETHYL LEAD ICSC: 0008
Novemba 2003

Tetraethyl plumbane
Lead tetraethyl
TEL
Risasi tetraethili
CAS # 78-00-2 Pb(C2H5)4
RTECS # TP4550000 Masi ya molekuli: 323.45
UN # 1649
EC # 082-002-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 93°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 93°C, uingizaji hewa.
Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutapika. Udhaifu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Degedege. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutapika. Udhaifu. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 61-26/27/28-33-50/53-62
S: 53-45-60-61
Angalia: [A, E; bidhaa ya kibiashara: angalia 1]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1649
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 3;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi. Weka gizani. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TETRAETHYL LEAD ICSC: 0008
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KINATACHO KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, asidi, halojeni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia mpira, aina fulani za plastiki na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (kama risasi) 0.1 mg/m³; (ngozi); A4; (ACGIH 2003).
MAK: (kama risasi) 0.05 mg/m³; H; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kupoteza fahamu. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Inaweza kusababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 200°C
Kiwango myeyuko: -136.8°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.7
Umumunyifu katika maji: ni dhaifu
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.027
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 8.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 93°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: zaidi ya 110°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-?
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.15
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Risasi tetraethili inayotumika kama msombo wa kuzuia kunaki katika petroli pia ina dibromidi ethilini na dikloridi ethilini kama taka. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Uhusiano baina ya harufu na kikomo cha mfiduo wa kazi hauwezi kuonyeshwa. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005