PHOSGENE ICSC: 0007
Oktoba 2002

Carbonyl chloride
Chloroformyl chloride
(silinda)
CAS # 75-44-5 COCl2
RTECS # SY5600000 Masi ya molekuli: 98.9
UN # 1076
EC # 006-002-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kubanwa kifua. Kuumwa koo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
Vua nguo zilizosibikwa. UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 26-34
S: (1/2-)-9-26-36/37/39-45
Angalia: [5]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 8

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1076
Msimbo wa NFPA: H 4; F 0; R 1;
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Weka mbali na sehemu ya kufanyia kazi. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PHOSGENE ICSC: 0007
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 300°C inapogusana na maji na unyevu, huzalisha gesi zenye sumu na babuzi (monoksidi kaboni na kloridi hidrojeni). Humenyuka pamoja na alumini, alkoholi isopropili.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm kama TWA; (ACGIH 2002).
EU OEL: 0.02 ppm, 0.08 mg/m³, kama TWA;
0.1 ppm, 0.4 mg/m³, kama STEL; (EU 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 8°C
Kiwango myeyuko: -118°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.4
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 161.6
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005