| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kuumwa kichwa. Kutokwa damu puani.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuumwa koo. Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. (Tazama Vidokezo).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. or bentonite clay in water, or Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T+, N R: 24/25-26-36/37/38-48/25-50/53 S: (1/2-)-22-28-36/37/39-45-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT7-I
|
Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Kilichofungwa vizuri. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO RANGI, RISHAI AU PODA FUWELE NYEUPE HADI MANJANO, RISHAI. MMUMUNYO WA DIKLORIDI YA PARAQUAT NA MAJI NI MWEKUNDU SANA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 300°C huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni, kloridi hidrojeni. Hushambulia metali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: kama paraquat, sehemu pumuzi wa vumbi 0.1 mg/m³ (ACGIH 2004). TLV: kama paraquat 0.5 mg/m³ (ACGIH 2004). MAK: 0.1 ppm; kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya kiwango cha juu: I(1); (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza na inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mafigo, ini, njia ya utumbo, mfumo wa moyo na mishipa na mapafu kusababisha kuharibika kwa utendaji, vidonda vya tishu pamoja na kutoka damu na unyuzi wa mapafu (lung fibrosis). Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri kucha kusababisha kuharibika kwa kucha. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko (hutengana): 300°C Kiwango myeyuko: 175-180°C Uzito wiani (maji = 1): 1.25 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 70 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <0.0001 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -4.2 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Maelezo kuhusu sumu ni kama na paraquati (CAS 4685-14-7). Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Dalili ya unyuzi wa mapafu (kushindwa kupumua, kupumua kwa nguvu) hazijitokezi mpaka baada ya siku nyingi. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||