METHYL ISOCYANATE ICSC: 0004
Novemba 2003

Isocyanatomethane
Isocyanic acid, methyl ester
CAS # 624-83-9 CH3NCO
RTECS # NQ9450000 Masi ya molekuli: 57.1
UN # 2480
EC # 615-001-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na maji, asidi, besi, vioksidishaji.
Povu linalokinza alkoholi, mchanga mkavu, Poda, dioksidi kaboni. USITUMIE vitenzi vya majimaji.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Mchomo.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Wekundu. Upofu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Zimua kioevu kilichomwagika kwa uangalifu kwa magadi. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Maunzi maalum.
Ainisho ya EU
Alama: F+, T+
R: 12-24/25-26-37/38-41-42/43-63
S: (1/2-)-26-27/28-36/37/39-45-63
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S2480
Msimbo wa NFPA: H 4; F 3; R 2; W
Isodhurika kwa moto. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL ISOCYANATE ICSC: 0004
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI VUKIVU CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha iwapo halisi. Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kukanza na kwa kuathiriwa na metali na vichocheo. Dutu hii hutengana inapogusana na maji. Dutu hii hutengana kwa haraka inapogusana na asidi na besi huzalisha gesi zenye sumu (sianidi hidrojeni, oksidi za nitrojeni, monoksidi kaboni). Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.02 ppm, 0.05 mg/m³; (ngozi); (ACGIH 2003).
MAK: 0.01 ppm, 0.024 mg/m³; Sh; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi yenye mvuke huu kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji. Husababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 39°C
Kiwango myeyuko: -80°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.96
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 54
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.44
Kiwango cha kumweka: -7°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 535°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.3-26
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji na vitenzi hidrati. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005