LEAD CHROMATE ICSC: 0003
Oktoba 2002

Plumbous chromate
Chromic acid, lead (II) salt (1:1)
CAS # 7758-97-6 PbCrO4
RTECS # GB2975000 Masi ya molekuli: 323.2
UN # 3288
EC # 082-004-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE! ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ona ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika au zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 61-33-40-50/53-62
S: 53-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-III
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LEAD CHROMATE ICSC: 0003
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE MANJANO HADI RANGI YA MACHUNGWA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi ya risasi. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali kama vile peroksidi hidrojeni. Humenyuka pamoja na alumini dinitronaftalini, feri(III) heksasianoferrati(IV). Humenyuka pamoja na vikaboni iwapo na halijoto kubwa kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: kama Pb 0.05 mg/m³ (kama TWA); A2; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
TLV: kama Cr 0.012 mg/m³ (kama TWA); A2; (ACGIH 2004.
MAK: Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake au vumbi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi na vidonda wa muda mrefu. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu. Dutu hii huweza kuathiri damu, uboho, mfumo mkuu wa neva, mfumo wa neva wa pembeni na mafigo kusababisha anemia, madhara kwa ubongo (kama kifafa), ugonjwa wa neva wa pembeni, tumbo kuuma na kuharibika kwa figo. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Inaweza kusababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana)
Kiwango myeyuko: 844°C
Uzito wiani: 6.3 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.0000058
DATA YA MAZINGIRA
Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mfano kufuata mwishono wa vyakula kwa samaki, kwa mimea, kwa mamalia.
VIDOKEZO
Krometi yaweza kusababisha kansa kwa binadamu, hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii. Pigimenti ya krometi risasi yaweza kuwa na kiwango kiasi misombo ya risasi mumunyifu katika maji. Mafusho yenye sumu (misombo ya risasi na kromiamu) hutokea wakati wa kuchomea vyuma, kukata na kukanza vitu vilivyowekewa krometi risasi. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Krometi risasi hutokea kiasili kama madini crocoite, phoenicochroite. Chrome yellow, Cologne yellow, King's yellow, Leipzig yellow, Paris yellow, C.I. Pigment yellow 34, C.I. 77600 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005