HYDROGEN ICSC: 0001
Machi 2002

(silinda)
CAS # 1333-74-0 H2
RTECS # MW8900000 Masi ya molekuli: 2.0
UN # 1049
EC # 001-001-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizio wa maji, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. Usishike silinda na mikono yenye mafuta.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Msongo wa hewa.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Jamidi kali.
Glavu za kuhami baridi.
Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwani ya usalama.

Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji.
Ainisho ya EU
Alama: F+
R: 12
S: (2-)-9-16-33
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1049
Msimbo wa NFPA: H 0; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
HYDROGEN ICSC: 0001
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ILIYOBANWA ISO HARUFU, ISO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. Gesi ni nyepesi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na hewa, oksijeni, halojeni na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Vichocheo vya metali, kama vile platina na nikeli, zinaongeza sana kasi ya mimenyuko hii.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: Kinacho nyima pumzi sahili (ACGIH 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kinacho nyima pumuzi sahili. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -253°C
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.07
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 500-571°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 4-76
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Pima kiwango cha hidrojeni na kigunduzi cha gesi kinachofaa (kigunduzi cha kawaida cha gesi inayowaka hakifai).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005